UTANGULIZI

Nina heshima kubwa ya kuwasilisha maoni yangu binafsi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusiana na namna na jinsi nchi zetu mbili, Zanzibar na Tanganyika, zinazounda Jamhuri ya Muungano zinavyopaswa kuongozwa kupitia mfumo mpya wa kikatiba utakaopatikana baada ya kukamilika mchakato unaoendelea sasa wa kupata Katiba Mpya. 413 more words